ROMA - Teremsha Bunduki (Official Audio) 🎶 | Catchy Swahili Song with Powerful Lyrics

Listen to ROMA's latest hit 'Teremsha Bunduki' featuring captivating beats and meaningful lyrics. Perfect for fans of Afrobeat and Swahili music. Don't miss out!

ROMA - Teremsha Bunduki (Official Audio) 🎶 | Catchy Swahili Song with Powerful Lyrics
VIVAROMA
1.2M views • Oct 20, 2025
ROMA - Teremsha Bunduki (Official Audio) 🎶 | Catchy Swahili Song with Powerful Lyrics

About this video

Intro

Ambaa weee x 8

Ambaaaa weeenaa x 4

Chorus

Afande teremsha bunduki/

Unaowatetea mbona hawakukumbuki/

Unatuonea unatupiga mabuti/

Mara virungu mara unataka kutushuti/ Eeeeee

*2

*Hook*

Afande teremshaaaaaa
(Haaaaai Haii Haii)

Afande teremsha bunduki (Haii Haii)

*4


*Verse 1*

Anaye andamana hana sindano wala kiwembe/

So kumuua muandamanaji sio ushujaa huo ni uzembe/

Mnabeba silaha nzito akili zenu zisiwe nyepesi/

Jeshi ni wito sio muujiza wa kupuliza gesi/

Nyie mnavunja amani/
Mnapiga raia mahakamani/
Mwisho wapoteze imani/
Waamue kumalizana mtaani/

Hamuheshimu muhimili/
Nyie makatili hamna maadili/
Hamstahili injili/
Labda albadir tena alfajiri/

Wanaofaidika boss zenu sio nyie askari wa chini/

Kwa posho ndogo mnatumwa mtupige sasa kwanini/

Yaani unamuua anayepambania kesho bora ya mwanao/

Huku unamlinda anayekuibia na ukistaafu hakupi mafao/

Watoto wao wana mali/
Wanaendesha bugatti ferrari/
We askari chakari/
Unadaiwa kwa mangi sukari/
Na hauna gari/
Tunagombania mwendokasi ni hatari/
Tukidai mabasi unatupiga risasi we ndo’ muasi/

Hook


*Verse 2*

Unayemuona adui unampiga ndio anaekulipa mshahara/

Ndio mwalimu wa mwanao ndio nesi aliyekufanyia tohara/

Ungana nasi hizo bunduki sio za kumlinda mtawala/

Anayetuibia na kututeka huku akihubiri 4R/

Tuna jobless laki tano anaahidi ajira elfu saba/

Na mnashangilia october mtatiki mtapigwa mnada/

Kama ameshindwa miaka minne ndio ataweza siku mia/

Kafeli bima mnadanganywa kitoto nawahurumia/

Hawaheshimu hata wajumbe ndio chanzo cha hizi vurugu/

Maana wanapitisha wabunge ambao wanaweza kuwamudu/

Tusiruhusu huu uchaguzi/
Ni uchafuzi na ulanguzi/
Wa kipuuzi mashuzi/
Wame-loose fuse/
Wamekata pumzi

*Chorus*

*Hook*

Video Information

Views

1.2M

Likes

60.7K

Duration

4:09

Published

Oct 20, 2025

User Reviews

4.8
(246)
Rate:

Related Trending Topics

LIVE TRENDS

Related trending topics. Click any trend to explore more videos.